Blog hii imezinduliwa nchini Tanzania kuonyesha harakati zote za hapa na pale za Mh.Angella Kizigha.
Monday, October 18, 2010
MHE.DR.JAKAYA MRISHO KIKWETE AITEKA KAWE.DAR
Mhe.Dr.Jakaya Mrisho akihutubia kawe, awaomba wananchi kuichagua CCM kwa kuwa iliahidi na ikatekeleza.katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika viwanja vya Tanganyika Packers huko Kawe.
Mhe.Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akimnadi Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Kawe Mhe.Angela Charles Kizigha katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika viwanja vya Tanganyika Packers huko Kawe.
Mhe.Angela Charles Kizigha akiwaomba ridhaa Wananchi wa Jimbo la kawe kukichagua chama cha Mapinduzi , pia aliwaambia Wananchi watakapo mchagua atajenga hospital kwa ajili ya jimbo hilo, akitoa mfano kwa mbunge iddi Azzan anayo Hospitali ya Mwananyamala ipo katika Jimbo lake la Kinondoni, kwa hiyo na yeye atajenga ili kuipunguzia mzigo Hospitali hiyo.
Mhe.Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akimnadi Bw. Othman, Mgombea Udiwani wa kata ya kawe kwa niaba ya madiwani wote wa Jimbo hilo la Kawe.


ambaye pia alitangaza kujiengua CUF
Wah. Juma Othman Juma na Fatma Maghimbi wakifurahia kujiunga na CCM.


Mhe.Angela Kizigha akizungumza kitu na Mgombea Udiwani wa kata ya Makumbusho Ndugu. Mutayoba.(Kusho kwenye Picha).
Mhe.Angela Kizigha akiwa katikati ya kundi la watu baada ya Mkutano kumalizika.
Watu walikuwa Nyomi hapatoshi.
Friday, October 15, 2010
MGOMBEA MWENZA URAIS WA CCM DR BILAL AKIHITIMISHA WIKI YA UWT PAMOJA NA KUWANADI WAGOMBEA UBUNGE NA UDIWANI WA WILAYA KINONDONI, DAR-ES-SALAAM
Mgombea mwenza Dr. Mohammed Gharib Bilali alihitimisha wiki ya UWT katika viwanja vya Mwinjuma kata ya Makumbusho, Kinondoni.alisema Chama Cha Mapinduzi kinajivunia umoja huo wa UWT kwani ni moja ya nguzo imara katika chama hicho.
Dr. Mohammed Gharib Bilali akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kawe Mh. Angela Kizigha katika uwanja wa mkutano wa wiki ya wanawake UWT uliofanyika kinondoni uwanja wa Mwinjuma.
Dr. Mohammed Gharib Bilal akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni Mh. Iddi Azzan wakati wa kuhitimisha wiki ya UWT.Mgombea Ubunge Jimbo la Ubungo Mh. Hawa Ngumbi akinadiwa na Dr Mohammed Gharib Bilali katika wiki ya wanawake ya UWT.
Ndugu Leila Seif ambaye alikuwa Mjumbe wa baraza la wanawake Taifa kupitia Chama cha CUF arudisha kadi CCM kwa Mheshimiwa Dr. Mohammed Gharib Bilal. wakati wa mkutano wa UWT, uliofanyika viwanja vya Mwinjuma, Kinondoni.
Subscribe to:
Posts (Atom)