Friday, October 15, 2010

MGOMBEA MWENZA URAIS WA CCM DR BILAL AKIHITIMISHA WIKI YA UWT PAMOJA NA KUWANADI WAGOMBEA UBUNGE NA UDIWANI WA WILAYA KINONDONI, DAR-ES-SALAAM

Mgombea mwenza Dr. Mohammed Gharib Bilali alihitimisha wiki ya UWT katika viwanja vya Mwinjuma kata ya Makumbusho, Kinondoni.alisema Chama Cha Mapinduzi kinajivunia umoja huo wa UWT kwani ni moja ya nguzo imara katika chama hicho.


Pia aliupongeza umoja huo kwa juhudi kubwa ya kuwakomboa wakinamama, na kuhakikisha wakinamama wanapata maendeleo na huduma zote muhimu, moja ya huduma hizo ni kupata mikopo yenye masharti ya unafuu zaidi. Na alimpongeza Mh. Jakaya Mrisho kikwete kwa kufungua benki ya wakinamama ili iwasaidie kwa maendeleo yao na kulisimamia taifa lao kwa uzuri zaidi.

Mwisho alimuombea kura Mgombea Urais Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete na kuwanadi wagombea Ubunge wote wa wilaya ya kinondoni pamoja na madiwani.
Dr. Mohammed Gharib Bilali akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kawe Mh. Angela Kizigha katika uwanja wa mkutano wa wiki ya wanawake UWT uliofanyika kinondoni uwanja wa Mwinjuma.
Dr. Mohammed Gharib Bilal akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni Mh. Iddi Azzan wakati wa kuhitimisha wiki ya UWT.
Mgombea Ubunge Jimbo la Ubungo Mh. Hawa Ngumbi akinadiwa na Dr Mohammed Gharib Bilali katika wiki ya wanawake ya UWT.
Ndugu Leila Seif ambaye alikuwa Mjumbe wa baraza la wanawake Taifa kupitia Chama cha CUF arudisha kadi CCM kwa Mheshimiwa Dr. Mohammed Gharib Bilal. wakati wa mkutano wa UWT, uliofanyika viwanja vya Mwinjuma, Kinondoni.

No comments:

Post a Comment