Monday, October 18, 2010

MHE.DR.JAKAYA MRISHO KIKWETE AITEKA KAWE.DAR

Mhe.Dr.Jakaya Mrisho akihutubia kawe, awaomba wananchi kuichagua CCM kwa kuwa iliahidi na ikatekeleza.katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika viwanja vya Tanganyika Packers huko Kawe.
Mhe.Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akimnadi Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Kawe Mhe.Angela Charles Kizigha katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika viwanja vya Tanganyika Packers huko Kawe.
Mhe.Angela Charles Kizigha akiwaomba ridhaa Wananchi wa Jimbo la kawe kukichagua chama cha Mapinduzi , pia aliwaambia Wananchi watakapo mchagua atajenga hospital kwa ajili ya jimbo hilo, akitoa mfano kwa mbunge iddi Azzan anayo Hospitali ya Mwananyamala ipo katika Jimbo lake la Kinondoni, kwa hiyo na yeye atajenga ili kuipunguzia mzigo Hospitali hiyo.
Mhe.Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akimnadi Bw. Othman, Mgombea Udiwani wa kata ya kawe kwa niaba ya madiwani wote wa Jimbo hilo la Kawe.
JK akijiandaa kumkabidhi Mh. Fatma Maghimbi kadi ya CCM baada ya kutangaza kujiengua chama cha wananchi CUF katika mkutano wa kampeni katika viwanja vya Tanganyika Packers vya Kawe.
JK akimkabidhi kadi ya CCM Mh. Juma Othman Juma
ambaye pia alitangaza kujiengua CUF
Wah. Juma Othman Juma na Fatma Maghimbi wakifurahia kujiunga na CCM.
JK akiongea na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Mh. John Guninita, Mwenyekiti wa kampeni wa CCM Mh Abdulrahman Kinana na wasaidizi wake wengine
Mhe.Angela Kizigha akisalimiana na baadhi ya wagombea waliohudhuria mkutano huo, akiwemo Mhe.Iddi Azzan Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni (kulia kwenye Picha)
Mhe.Angela Kizigha akizungumza kitu na Mgombea Udiwani wa kata ya Makumbusho Ndugu. Mutayoba.(Kusho kwenye Picha).
Mhe.Angela Kizigha akiwa katikati ya kundi la watu baada ya Mkutano kumalizika.
Watu walikuwa Nyomi hapatoshi.
Msanii Diamond akiburudisha umati huo
Vijana machachari wa Tip Top Connection wakifanya vitu vyao leo Kawe

No comments:

Post a Comment